Mrembo
Eveline katika picha ya pamoja na wenzake waliotwaa tatu bora, ambapo
kwa upande wa kushoto ni Happy Tarmo na kulia ni Merry Joel.
Mrembo
Evelini Baasa ( aliyekaa) akiwa na washiriki wenzake Hapy Tarimo
kushoto na Merry Joel Kulia, Na wa kwanza kushoto ni aliyekuwa
mwakilishi wa mgeni rasmi Adam Akyoo, na wa mwisho kulia ni diwani wa
Karatu mjini Jublet Mnyenye.
Mlimbwende
Eveline Baasa akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo
wakiongozwa na jaji mkuu Faustine Mwandago ( watatu kutoka kulia
aliyvalia shati la mistari).
warembo,
wakionyesha vazi la usiku kwa pamoja ambapo wa kwanza kulia ni Eveline
Baasa, anaefuata ni merry joel, Asha Bonivenrute, Upendo Mtweve,
Veronika Joel, Scolastika Fransis, Janeth Jackson, Glorry Aloyce, Happy
Tarimo.
======== ======= =======
Na Bertha Ismail - Arusha.
Mrembo
Eveline Baasa (19) amefanikiwa kutwaa taji ya Ulimbwende wa wilaya ya
Karatu kwa mwaka 2014 na kuwabwaga wenzake wanane katika kinyanganyiro
kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro Camp uliopo mjini hapa.
Eveline
amekua mrembo wa kwanza kwa wilaya hiyo tangu kuanzishwa kwa wilaya ya
karatu ambapo alibahatika kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano na
pia kuingia katika shindano la miss Arusha linalotarajiwa kufanyika
mwezi june sambamba na hilo amepata udhamini wa maandalizi yote kwa
ajili ya kushiriki shindano lililoko mbele yake.
Mshindi
wa pili alikuwa Happy Tarmo (19) ambaye alijinyakulia fedha taslim
shilingi laki tatu na kufuatiwa na Merry Joel (21) aliyezawadiwa
shilingi laki mbili na mshindi wa nne ikienda kwa Veronica John (21) na
washiriki wenzake watano ambapo alipata kifuta jasho cha shilingi elfu
themanini kila mmoja.
Hili
lilikuwa shindano la kwanza kwa wilaya ya Karatu ambalo lilikuwa
kivutio kikubwa kwa wakazi wa wilaya hiyo kufuatia ushindani mkubwa
uliojitokeza kwa washiriki wote kuwa na sifa zote hali iliyowapa kazi ya
ziada majaji waliokuwa wakiongozwa na mratibu wa miss kanda ya
kaskazini Faustine Mwandago.
Mashabiki
wa tasnia ya urembo mjini Karatu waliokuwa wakiongozwa na diwani wa
Karatu mjini Jubilate Mnyenye walilipuka kwa shangwe baada ya jaji mkuu
Mwandago kumtangaza mlimbwende Evaline kuwa ndiye mshindi wa miss
Karatu 2014 matokeo yaliyoungwa mkono na wadau wote wa tasnia ya urembo
waliohudhuria onyesho hilo.
Hili
linakuwa shindano la kwanza kwa ngazi ya kitongoji cha wilaya ya Karatu
kwa mkoa wa Arusha wenye vitongoji vitatu ambavyo ni Karatu, Monduli na
kituo cha Arusha mjini ( Arusha city center).
Aidha
baada ya kitongoji cha Karatu kumpata mrembo wake, wiki ijayo
kinyang’anyiro cha pili kitafanyika kitongoji cha monduli na kitongoji
cha mwisho kitakua cha arusha city kitakachofanya baadae mwaka huu
ikiwa ni mchakato wa kumpata miss Arusha.
Aidha
kila kitongoji kitatoa warembo wane kila kitongoji ambapo kutakuwa na
jumla ya warembo 12 ambapo watashiriki katika kinyanganyiro cha kumsaka
mrembo wa mkoa wa Arusha
Mgeni
rasmi katika shindano hilo la miss Karatu alikua ni mhifadhi mkuu wa
mamlaka ya Ngorongoro Fredy Manongi ambaye aliwakilishwa na afisa
uhusiano wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongo Adam Akyoo ambaye aliwataka
warembo kutumia fursa walionayo kupambana na ujangili kwa kutoa taarifa
za watu wanajishughulisha na ujangili.
Akyoo
alisema kuwa kupambana na ujangili siyo lazima kushika mitutu ya
bunduki kumzuia mwindaji bali utoaji wa elimu pia unaweza kusaidia
kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la ujangili nchini.
Kwa
upande wake diwani wa karatu mjini, Jublet Mnyenye alisema kuwa
amefurahishwa na waandaji wa kinyang’anyiro hicho cha kumsaka mlimbwende
wa Karatu pia karatu mjini kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya
kwanza wilayani humo ambapo ameahidi kusapoti mashindano hayo mara
nyingine yatakapofanyika kwa kujitolea ukumbi, zawadi za washindi pamoja
na maandalizi yote kwa ujumla.
Kinyanganyiro
hicho cha aina yake kilidhaminiwa na Makampuni mbalimbali na wadau wa
urembo wilayani humo wakiwemo kinywaji cha Redd’s, ZARA tour, hifadhi
ya mamlaka ya Ngorongoro, Beauty point Cosmetics pamoja na mdau wa
ulimbwende Mh, Steven Siay.