Pages

Ads 468x60px

Featured Posts

Monday, September 22, 2014

TUNDA MAN ASINDIKIZA SHOW YA VIPAJI WAREMBO MISS TANZANIA BABATI MKOANI MANYARA


 Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini.Na Father Kidevu Blog
 Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.

Wednesday, May 28, 2014

THIS IS HIPHOP NDANI YA ARACHUGA TAR 31.05.2014 SI YA KUKOSAAA!!!!!!!!!!!!!!!!

Show ya "This is HipHop" Usiku wa Saturday 31st May 2014 pale VIA VIA kwa elfu 5 tu! Appearance za kutosha, Watengwa,Lavosti, Moplus, Vatoloco, Nako2Nako,Songa na Wengine Kibao. Support Artists Wa HomeGround

Friday, May 2, 2014

MREMBO EVELINE BAASA ATWAA TAJI LA ULIMBWENDE WILAYA YA KARATU KWA MWAKA 2014

 Mrembo Eveline katika picha ya pamoja  na wenzake waliotwaa tatu bora, ambapo kwa upande wa kushoto ni Happy Tarmo na kulia ni Merry Joel.
 Mrembo Evelini Baasa ( aliyekaa) akiwa na washiriki wenzake Hapy Tarimo kushoto na Merry Joel Kulia, Na wa kwanza kushoto ni aliyekuwa mwakilishi wa  mgeni rasmi Adam Akyoo, na wa mwisho kulia ni diwani wa Karatu mjini Jublet Mnyenye.
Mlimbwende Eveline Baasa akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na jaji mkuu Faustine Mwandago ( watatu kutoka kulia aliyvalia shati la mistari).
  warembo, wakionyesha vazi la usiku kwa pamoja ambapo wa kwanza kulia ni Eveline Baasa, anaefuata ni merry joel, Asha Bonivenrute,  Upendo Mtweve, Veronika Joel, Scolastika Fransis, Janeth Jackson, Glorry Aloyce, Happy Tarimo.
========  =======  =======
Na Bertha Ismail - Arusha.
Mrembo Eveline Baasa (19) amefanikiwa kutwaa taji ya Ulimbwende wa wilaya ya Karatu kwa mwaka 2014 na kuwabwaga wenzake wanane katika kinyanganyiro kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro Camp uliopo mjini hapa.

Eveline amekua mrembo wa kwanza kwa wilaya hiyo tangu kuanzishwa kwa wilaya ya karatu ambapo alibahatika kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano na pia kuingia katika shindano la miss Arusha linalotarajiwa kufanyika mwezi june sambamba na hilo amepata udhamini wa maandalizi yote kwa ajili ya kushiriki shindano lililoko mbele yake.

Mshindi wa pili alikuwa Happy Tarmo (19) ambaye alijinyakulia fedha taslim shilingi laki tatu na kufuatiwa na Merry Joel (21) aliyezawadiwa shilingi laki mbili na mshindi wa nne ikienda kwa  Veronica John (21) na washiriki wenzake watano ambapo alipata kifuta jasho cha shilingi elfu themanini  kila mmoja.

Hili lilikuwa shindano la kwanza kwa wilaya ya Karatu ambalo lilikuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa wilaya hiyo kufuatia ushindani mkubwa uliojitokeza kwa washiriki wote kuwa na sifa zote hali iliyowapa kazi ya ziada majaji waliokuwa wakiongozwa na mratibu wa miss kanda ya kaskazini Faustine Mwandago.

Mashabiki wa tasnia ya urembo mjini Karatu waliokuwa wakiongozwa na diwani wa Karatu mjini Jubilate Mnyenye walilipuka kwa shangwe baada ya jaji mkuu Mwandago kumtangaza mlimbwende Evaline kuwa ndiye  mshindi wa miss Karatu 2014 matokeo yaliyoungwa mkono na wadau wote wa tasnia ya urembo waliohudhuria onyesho hilo.

Hili linakuwa shindano la kwanza kwa ngazi ya kitongoji cha wilaya ya Karatu kwa mkoa wa Arusha wenye vitongoji vitatu ambavyo ni Karatu, Monduli na kituo cha Arusha mjini         ( Arusha city center).

Aidha baada ya kitongoji cha Karatu kumpata mrembo wake, wiki ijayo kinyang’anyiro cha pili  kitafanyika kitongoji cha monduli na kitongoji cha mwisho kitakua cha arusha city  kitakachofanya baadae mwaka huu ikiwa ni mchakato wa kumpata miss Arusha.
  
Aidha kila kitongoji kitatoa warembo wane kila kitongoji ambapo kutakuwa na jumla ya warembo 12 ambapo watashiriki katika kinyanganyiro cha kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha

Mgeni rasmi katika shindano hilo la miss Karatu alikua ni mhifadhi mkuu wa mamlaka ya Ngorongoro Fredy Manongi ambaye aliwakilishwa na afisa uhusiano wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongo Adam Akyoo ambaye aliwataka warembo kutumia fursa walionayo kupambana na ujangili kwa kutoa taarifa za watu wanajishughulisha na ujangili.

Akyoo alisema kuwa kupambana na ujangili siyo lazima kushika mitutu ya bunduki kumzuia mwindaji bali utoaji wa elimu pia unaweza kusaidia kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la ujangili nchini.

Kwa upande wake diwani wa karatu mjini, Jublet Mnyenye alisema kuwa amefurahishwa na waandaji wa kinyang’anyiro hicho cha kumsaka mlimbwende wa Karatu pia karatu mjini kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza wilayani humo ambapo ameahidi kusapoti mashindano hayo mara nyingine yatakapofanyika kwa kujitolea ukumbi, zawadi za washindi pamoja na maandalizi yote kwa ujumla.

Kinyanganyiro hicho cha aina yake kilidhaminiwa na Makampuni mbalimbali na wadau wa urembo wilayani humo wakiwemo  kinywaji cha Redd’s, ZARA tour, hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro, Beauty point Cosmetics pamoja na mdau wa ulimbwende Mh, Steven Siay.

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

  

         


Tuesday, March 4, 2014

Breaking News, Lord Eyes Amesimamishwa Kazi Ndani Ya Kampuni Ya Weusi


 
Nikki Wa Pili Msemaji Wa Weusi Kampuni amesema Leo mchana kuwa rapper Lord Eyes Amesimamishwa Kazi na Kampuni hio na taarifa zaidi zitatolewa muda ukifikia.
Nikki Amefunguka kuwa Lord Eyes asihusishwa na Kazi za Weusi na Weusi wasihusishwa na Lord Eyes.
Taarifa za Lord Eyes Aulizwe mwenyewe na sio Weusi.